Wakaazi wa kijiji kimoja mjini Kakamega wameshangazwa na kisa ambacho barobaro mmoja ameamua kujichimbia kaburi mbele ya nyumba yake huku akidai kuwa amechoshwa na maisha.
Kulingana na mdokezi wetu jamaa huyo kwa jina Fredrick Mumeyu almaarufu Holiday amekuwa akilalama kuwa maisha yamekuwa magumu kutokana na gharama ya maisha kupanda.
“Maisha imekuwa ngumu, bei ya bidhaa inapanda kila kuchao, kupata kazi imekuwa changamoto kubwa ni heri kujitoa mapema kabla ya gharama kukuwa ghali zaidi,” alisema Mumeyu.
Kulingana na jamaa zake, barobaro huyo pia amejinunulia jeneza analodai kuwa ni nzuri na linamfaa.
“Tumekuwa tukisikia tu watu hujichimbia kaburi leo tumeona na macho yetu. Ni jambo la kusikitisha kuona mtu mzima mwenye akili zake akijichimbia kaburi. Hata jana alionekana kwa muhudumu mmoja mjini kakamega akijipima ndani ya jeneza,” alisema mmoja wa wakaazi.
Read: Mwanaume Ajinyonga Kakamega Baada Ya Kutorokwa Na Mke
Kulingana na mila na tamaduni za jamii ya Waluhya ni mwiko kwa mtu kufanya kitendo kama hicho na anapaswa kufanyiwa tambiko itakayohusisha kuchinjwa kwa kondoo pamoja na kupewa dawa za kienyeji ili kuondoa laana katika jamii hiyo.
“Huyu kijana analeta laana kubwa sana kwa familia, itabidi amefanyiwa tambiko itakayohusishwa kuchinja kwa kondoo pamoja na kumtakasa kwa madawa ya kienyeji ili kutoa mazimwi yanayomwandama la si hivyo kuna mtu katika hii jamii hata kama si yeye atajitoa uhai,” alisema Mzee Nicholas, kutoka katika kijiji hicho.
Inaripotiwa kuwa Holiday anaendelea kulinadhifisha kaburi lake huku wazee wa kijiji wakiwaonya wenyeji dhidi ya kumtisha kutoka kwa kazi yake.
Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu