Menu
in ,

Tanzania Yabatilisha Sherehe Za Siku Ya Wanawake Duniani, Yavitaka Vyama Pinzani Kujiunga Na Serikali Katika Maadhimisho Rasmi

Serikali ya Muungano wa Tanzania imebatilisha sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika mikoa miwili, na kuviomba vyama andalizi kujiunga na serikali katika maadhimisho rasmi.

Sherehe hizo zilikua zimeandaliwa na chama cha Chadema katika Mkoa wa Geita na Act Wazalendo katika Mkoa wa Katavi.

Aidha, barua kutoka wakuu wa jeshi la polisi la mikoa yote miwili zilizolifikia chapisho la Kahawa Tungu zimewataka wakuu wa vyama hivyo kuweka kando mipangilio yao na badala yake kujiunga na serikali kuadhimisha siku hiyo.

Read: Indo Solutions Yashutumiwa Baada Ya Kukiuka Mkataba Wa Korosho Na Nchi Ya Tanzania

“Kwa barua hii ninawazuia kufanya maadhimisho hayo katika ukumbi wa Moyo wa Huruma na badala yake wanawake wote waungane na wanawake wenzao katika maeneo hayo yaliyotajwa kiserikali. Hii ni pamoja na kuzuia kufanya matangazo yoyote yanayohusiana na kufanya maadhimisho hayo kwa itikadi za kanisa,” alisema Ally A Kitumbu, Mkuu wa Polisi wa Geita.

 

 

Hali ilikua hiyo hiyo katika Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Mpanda ambapo mkuu wa polisi katika wilaya hito alisema: “Kwa kuwa ni siku ya kitaifa ya wanawake haitawezekana kuwepo makundi mawili katika maadhimisho hayo. Nawashauri tuungane pamoja siku hiyo kimkoa au mnaweza kufanya siku moja kabla ya tarehe 08/03/2019 au baada ya tarehe hiyo.”

Wa aidha, kiongozi wa Chama cha Act Wazalendo Zito Kabwe Ruyagwa ametaja kitendo hicho kama dalili za udikteta kutoka kwa Raisi John Pombe Magufuli.

“The letters seems similar contentwise signifying ‘orders from the top’ (Barua hizi zinafanana katika yaliyomo, zikiashiria ‘amri kutoka juu’,” alisema Kabwe katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu

Written by Francis Muli

Follow me on Twitter @francismuli_ Email: Editor@Kahawatungu.com

Leave a Reply

Exit mobile version