Site icon KahawaTungu

Rais Magufuli Atoa Shilingi Milioni 200 Kufadhili Kituo Cha Redio Cha Magic FM, Kinachomilikiwa Na CCM

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. [PICHA/ KWA HISANI]
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amehaidi shilingi milioni 200 (Ksh 8.6 milioni) kwa ajili ya kufadhili ununuzi wa vifaa vipya vya kituo cha redio cha Magic FM.

Kituo hicho kinamilikiwa na shirika la Africa Media Group (AMG) ambalo linamilikiwa na chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akitoa ufadhili huo Rais Magufuli amewarai wanahabari wa kituo hicho kuzalisha maudhui ambayo yatawasaidia Watanzania yakiwemo kilimo, biashara, ufugaji na uvuvi.

“Nataka Africa Media Group Ltd iwe na vyombo vyenye nguvu vinavyotazamwa kila mahali hapa nchini hadi nje ya nchi. Tanzania haiwezi kuwa soko la kuangalia vyombo vya kutoka nje ya nchi. Watu waangalie vyombo vya habari vya nje lakini vyombo vyetu viwe ndio mwongozo wa maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 50,” alisema Magufuli.

Aidha Dkt Magufuli amehakikishia wananchi wake kwamba nchi inasonga vyema kiuchumi na huduma za kijamii kama vile afya, elimu, maji, nishati na miundombinu ya usafiri.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Magufuli amewarai raia kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na dhuluma na utumizi mbaya wa rasilimali za taifa.

Read: Trans Nzoia MCA Phyllis Njeri Arrested For Drunk Driving With Child On Board

Katika ziara yake mjini Dar-es-Salaam ambako alizuru miradi kadhaa ya CCM, Rais Magufuli ameshikilia kwamba serikali yake inaendelea kuutimiza wajibu wake wa kutetea Watanzania kwa ujumla.

Je, unayo habari ya kusisimua ambayo ungependa tuiandike? Itume kwenye barua pepe Editor@kahawatungu.com  ama WhatsApp +254707482874.

Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com
Exit mobile version