Kampuni ndogo kutoka Kenya ambayo ilijishindia kandarasi ya kununua korosho kutoka nchi jirani ya Tanzania bado haijafanya malipo yoyote mpaka sasa, hii ni kulingana na Kiongozi wa chama cha Wazalendo Zitto Kabwe Ruyagwa.
Kabwe Ruyagwa anadai kuwa Indo Power Solutions Ltd ambayo ilitarajiwa kulipa dola milioni mia moja na themanini nuka mbili ($180.2/TZS 400B)haijawasilisha pesa zozote kwa mujibu wa mkataba wa pamoja na LC Magumashi.
Akizungumza kupitia mtandao wa jamii wa Twitter siku ya Jumanne, Ruyagwa aidha alisema kuwa korosho bado hazijaweza kusafirishwa baada ya mabenki ambayo yalitarajiwa kufadhili shughuli hiyo kugoma.
“Ile Kampuni ‘hewa’ kutoka Kenya iliyoingia mkataba wa kununua Korosho tani 100K kwa US$180m (TZS 400b) mpaka sasa haijalipa pesa kwa mujibu wa mkataba pamoja na LC magumashi, ” Ruyagwa alisema.
“Korosho hazijabebwa na mabenki ya ndani yaliyofuatwa kutoa pesa yamegoma. Serikali ya CCM #Maarifaless.”
Ile Kampuni ‘hewa’ kutoka Kenya iliyoingia mkataba wa kununua Korosho tani 100K kwa US$180m (TZS 400b) mpaka sasa haijalipa pesa kwa mujibu wa mkataba pamoja na LC magumashi, Korosho hazijabebwa na mabenki ya ndani yaliyofuatwa kutoa pesa yamegoma. Serikali ya CCM #Maarifaless
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 19, 2019
Aliilaumu Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inayoongozwa na raisi John pombe Magufuli kwa kukosa kutoa mwongozo bora.
Madhara ya maamuzi fyongo Kuhusu Korosho pamoja na sera za hovyo za Uchumi. Gharama za kuagiza bidhaa kutoka nje ( mafuta, mashine na malighafi) zinakuwa kubwa sana ilhali mauzo yetu nje kiduchu. Serikali ya CCM inatoa kipaumbele kwenye UKATILI dhidi ya Watu,Uchumi chali pic.twitter.com/wdw0Lusefd
— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) February 19, 2019
Kampuni ya Indo Power Solutions ikiwakilishwa na mkurugenzi mtendaji Brian Mutembei iliingia katika mkataba wa kununua korosho kutoka kwa wakulima wa nchi ya Tanzania mnamo Januari 30 mwaka huu. Hii ni baada ya kuzipiku kampuni zingine nane zilizokuwa zimeonyesha nia katika biashara ya korosho.
Licha ya kampuni hiyo kutotambulika hau kuwa na uzoefu wa kununua au kuuza korosho ilipewa kandarasi hiyo.
Mkurugenzi wa bodi ya nafaka nchini Tanzania Hussein Mansour aliidhinisha mkutaba huo katika makao makuu ya Jumuia ya Afrika mashariki mjini Arusha.
Vile vile, waziri wa sheria Palamagamba Kabudi, waziri wa biashara Joseph Kakunda na gavana mkuu wa benki kuu ya Tanzania Florens Luoga ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla iyo.
Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu
Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874