Biwi la simanzi limeikumba familia moja kutoka kijiji cha Embwambwa eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega baada ya mwili wa mwanaume mmoja kupatikana ukininginia kwa kamba chumbani mwake.
Patrick Siteti, mwenye umri wa miaka 40, anadaiwa kujinyonga kwa kamba baada ya mkewe kumtoroka huku akimwachia mzigo wa kuwalea wanao.
Kulingana na mamake marehemu Salome Siteti, mwendazake aliamua kuchukua hatua hiyo baada yake kuachwa na mkewe kutokana na hali yao ya ufukara.
Soma: Burundi Yawaachilia Huru Wanafunzi Waliomkejeli Raisi Nkurunziza Kupitia Michoro
Inaripotiwa kuwa jambo hili lilimfanya kusongwa na mawazo, na mara kwa mara amekuwa akijaribu kujitoa uhai kabla yake kuokolewa na jamaa zake.
“Tangia kijana wangu abaki na upweke amekuwa akifanya vitu vya kushangaza, majuma kadhaa kabla ya tukio hili alijifungia kwa nyumba na kuiwasha moto kwa lengo la kujiteketeza lakini akaokolewa na ndugu zake kabla ya moto huo kuenea. Siku chache baadaye alijidunga kisu tumboni tukamkimbiza hospitalini. Amekuwa akisema amechoshwa na maisha na hawezi kuafiki majukumu yake kama baba wa familia,” alisema mamaye mwendazake.
Uchunguzi wa polisi unaendelea.
Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu
Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874