Shehena ya samaki wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili (TSh 60 milioni) kutoka China wameteketezwa katika dampo la Pugu Kinyamwezi Jijini Dar Es Salaam, Tanzania kwa madai ya kuwa na sumu.
Samaki hao ambao wanakisiwa kuwa takribani tani kumi na moja waliteketezwa mnamo siku ya Jumatatu baada ya kubainika kuwa wana madini ya Zebaki.
Kulingana na Mkurugenzi Msaidizi wa Ulinzi Rasilimali za Uvuvi, Nchama Marwa, madini hayo yana madhara kwa jamii na yana uwezo wa kusababisha Saratani na kuharibu uzazi.
Zoezi hilo lililosimamiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina, liliamrishwa baada ya Wizara yake kushinda kesi iliyokuwa imewasilishwa kupinga hatua iyo.
Wakishuhudia zoezi hilo, wamiliki wa shehena iyo, wameipongeza serikali kwa hatua hiyo na kuziomba taasisi za serikali kushirikiana ili kuwapunguzia hasara waliyoipata.
Mpaka sasa, vyombo vya habari kutoka nchi ya Tanzania vimebaini kuwa takriban tani 31 wa samaki wanaoingia nchini kutoka China wameteketezwa.
Inadaiwa kuwa, serikali imekaza kamba katika ukaguzi huo ili kuhakikisha kuwa samaki wanaoingia nchini ni salama kwa binadamu.
Aidha, serikali imewaomba wanainchi kuripoti visa vya samaki hatari kama hao kwa vituo vya usalama ili kulinda maisha ya binadamu.
Kando na Tanzania, visa vya samaki kutoka China pia vimeripotiwa nchini Kenya huku raisi Uhuru Kenyatta akikashifu hatua ya kuagiza samaki kutoka nje.
“Jameni tunatoa samaki kutoka China na wenzetu hapa… hata kama finance bill imepita, tunaweza sema hiyo samaki imeingia ni mbaya, kuna njia nyingi serikali inaezafanya kazi ndo tuhakikishe watu wetu wanafaidika,” Raisi Kenyatta alisema.
Licha ya madai ya raisi, duru za kuaminika zinaarifu kuwa samaki kutoka China ni wengi nchini.
Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu
Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874
GIPHY App Key not set. Please check settings
One Comment