Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    KahawatunguKahawatungu
    Button
    • NEWS
    • BUSINESS
    • KNOW YOUR CELEBRITY
    • POLITICS
    • TECHNOLOGY
    • SPORTS
    • HOW-TO
    • WORLD NEWS
    KahawatunguKahawatungu
    EAST AFRICA

    Burundi Yawaachilia Huru Wanafunzi Waliomkejeli Raisi Nkurunziza Kupitia Michoro

    Wycliffe NyamasegeBy Wycliffe NyamasegeMarch 27, 2019No Comments2 Mins Read
    Facebook Twitter WhatsApp Telegram Email
    Picha ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza iliyofanywa kejeli na wasichana hao. [PICHA/ KWA HISANI]
    Share
    Facebook Twitter WhatsApp Telegram Pinterest Email Copy Link

    Wanafunzi watatu waliotiwa mbaroni wiki iliyopita kwa tuhuma za kumkejeli raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza kupitia kwa michoro katika madaftari yao wameachiliwa huru.

    Kwa mujibu wa waziri wa haki wa nchi hiyo Bwana Aimee Laurentine Kanyana aliyekuwa akizungumza na wanahabari, wasichana hao wenye umri wa miaka 15, 16 na 17 wameachiliwa huru kwa sasa.

    Waziri huyo aliwaomba wazazi kuwaelekeza wanao vyema.

    “Tunawaomba wazazi kuwapa wanao mafunzo mema kwa kila wanachojishirikisha nacho. Kadhalika, ningependa kuwaonya wanafunzi wetu kuwa yeyote ambaye amefikisha umri wa miaka kumi na tano au zaidi anaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria iwapo atapatikana akifanya uhalifu wowote ule.” alisema Bwana Kanyana.

    Kukamatwa kwa wanafunzi hao kulikashifiwa katika mitandao ya kijamii haswa Twitter kwa kutumia hashitegi #FreeOurGirls.

    Wengi wanaamini kuwa mchango wao ndio uliopelekea wasichana hao wenye umri mdogo kuachiliwa.

    Kulikua na hofu kuwa wasichana hao wangefungwa gerezani kwa miaka mitano.

    Soma:Wanafunzi Watatu Nchini Burundi Wakabiliwa Na Kifungo Gerezani Kwa Kumchora Rais Nkurunziza Kikejeli

    Vyombo vya habari nchini Burundi viliripoti kuwa wanafunzi hao walikamatwa na wengine wanne, ambao waliachiliwa baadaye katika hali tatanishi.

    Sio mara ya kwanza nchi hiyo imejipata kwenye kurunzi la kimataifa kwa kuwakamata wanafunzi wanaokejeli kiongozi wa nchi.

    Mnamo mwaka wa 2016, vyombo vya dola nchini humo viliwakamata wanafunzi wanane wa shule ya sekondari kwa tuhuma za kumkashfu Rais baada ya kuchora michoro isiyofaa dhidi yake.

    Watetezi wa haki za kibinadamu nchini humo wamekashifu utawala wa Rais Nkurunziza kwa wanachokitaja kuwa unyanyasaji wa haki za wanafunzi wasiokubaliana na uongozi wake.

    Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu

    Email your news TIPS to Editor@Kahawatungu.com — this is our only official communication channel

    #FreeOurGirls Burundi Pierre Nkurunziza
    Follow on Facebook Follow on X (Twitter)
    Share. Facebook Twitter WhatsApp LinkedIn Telegram Email
    Wycliffe Nyamasege

    Email news@localhost

    Related Posts

    Reprieve as court lifts order baring Marie Stopes from offering abortion services

    December 19, 2025

    Kung’u Muigai stopped from publishing bribery claims against Justice Lenaola

    December 19, 2025

    Kasmuel McOure Joins Ministry of Cooperatives to Boost Youth Empowerment

    December 18, 2025

    Comments are closed.

    Latest Posts

    How To Draw Shadow

    December 19, 2025

    How To Draw Planets

    December 19, 2025

    How To Draw Peppa Pig

    December 19, 2025

    How To Draw On PC

    December 19, 2025

    Jane Kaczmarek Net Worth

    December 19, 2025

    Bradley Whitford Net Worth

    December 19, 2025

    Janel Moloney Net Worth

    December 19, 2025

    Ann Dowd Net Worth

    December 19, 2025
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    © 2025 Kahawatungu.com. Designed by Okii.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.