Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    KahawatunguKahawatungu
    Button
    • NEWS
    • BUSINESS
    • KNOW YOUR CELEBRITY
    • POLITICS
    • TECHNOLOGY
    • SPORTS
    • HOW-TO
    • WORLD NEWS
    KahawatunguKahawatungu
    NEWS

    Mwanaume Ajinyonga Kakamega Baada Ya Mke Kumtoroka

    KahawaTungu ReporterBy KahawaTungu ReporterApril 29, 2019Updated:April 29, 2019No Comments1 Min Read
    Facebook Twitter WhatsApp Telegram Email
    Suicide Photo | Courtesy
    Share
    Facebook Twitter WhatsApp Telegram Pinterest Email Copy Link

    Biwi la simanzi limeikumba familia moja kutoka kijiji cha Embwambwa eneo  bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega baada ya mwili wa mwanaume mmoja  kupatikana ukininginia kwa kamba chumbani mwake.

    Patrick Siteti, mwenye umri wa miaka 40, anadaiwa kujinyonga kwa kamba baada ya mkewe kumtoroka huku akimwachia mzigo wa kuwalea wanao.

    Kulingana na mamake marehemu Salome Siteti, mwendazake aliamua kuchukua hatua hiyo baada yake kuachwa na mkewe kutokana na hali yao ya ufukara.

    Soma: Burundi Yawaachilia Huru Wanafunzi Waliomkejeli Raisi Nkurunziza Kupitia Michoro

    Inaripotiwa kuwa jambo hili lilimfanya kusongwa na mawazo, na mara kwa mara amekuwa akijaribu kujitoa uhai kabla yake kuokolewa na jamaa zake.

    “Tangia kijana wangu abaki na upweke amekuwa akifanya vitu vya kushangaza, majuma kadhaa kabla ya tukio hili alijifungia kwa nyumba na kuiwasha moto kwa lengo la kujiteketeza lakini akaokolewa na ndugu zake kabla ya moto huo kuenea. Siku chache baadaye alijidunga kisu tumboni tukamkimbiza hospitalini. Amekuwa akisema amechoshwa na maisha na hawezi kuafiki majukumu yake kama baba wa familia,” alisema mamaye mwendazake.

    Uchunguzi wa polisi unaendelea.

    Email your news TIPS to Editor@kahawatungu.com or WhatsApp +254707482874. You can also find us on Telegram through www.t.me/kahawatungu

    Email your news TIPS to Editor@Kahawatungu.com — this is our only official communication channel

    Kakamega
    Follow on Facebook Follow on X (Twitter)
    Share. Facebook Twitter WhatsApp LinkedIn Telegram Email
    KahawaTungu Reporter
    • Website

    Email: Editor@Kahawatungu.com

    Related Posts

    M-Pesa attendant shot and wounded, robbed of Sh400,000 in Busia attack

    March 17, 2026

    Two suspects arrested, stolen police rifle recovered in Mombasa operation

    March 17, 2026

    Two people killed in Tana River after knife attack sparks mob justice

    March 17, 2026

    Comments are closed.

    Latest Posts

    KRA to Roll Out EAC Customs Bond on March 23

    March 17, 2026

    KPA Opens Internship Opportunities for Youths

    March 17, 2026

    Kenyatta and Maseno Universities Open Job Vacancies

    March 17, 2026

    M-Pesa attendant shot and wounded, robbed of Sh400,000 in Busia attack

    March 17, 2026

    Two suspects arrested, stolen police rifle recovered in Mombasa operation

    March 17, 2026

    Two people killed in Tana River after knife attack sparks mob justice

    March 17, 2026

    Probe as lorry is torched along Lokichar–Lokori road in Turkana

    March 17, 2026

    How to Plant Butternut Seeds

    March 17, 2026
    Facebook X (Twitter) Instagram Pinterest
    © 2026 Kahawatungu.com. Designed by Okii.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.